English

StraightBook Ilitengenezwa Na Muhandisi wa Program Wa Afrika Kuanzia Mwaka 2012 Hadi 2017

Umeshangaa? Ndio, Program Kubwa Kama Hii Iliweza Kutengenezwa Kwa Miaka 5 Mfululizo Na Mhandisi Wa Mifumo Ya Computer Mtanzania Aitwae Mr. Bukhary Kibonajoro (B.Sc in Computer Science, University of Dar es Salaam). Alianza Kuutengeneza Mwaka 2012 Baada Tu Ya Kumaliza Chuo Kikuu Ili Baadae Aanzishe Kampuni Ya Software Ambayo Ndio StraightBook Kwa Sasa. Hadi Sasa Bado Anaongoza Kundi La Wahandisi Wenye Vipaji Watengezaji Wa Mifumo Ya Computer Katika Kutengeneza Mfumo Huu Katika Kampuni Hii.



Mtu huyu hajatengeneza StraightBook pekee bali pia na mifumo mingine mikubwa kama:
1. Mfumo Wa Masuala Ya Fedha Na Taaluma Mashuleni: FreshFee
2. Mfumo Wa Masuala Ya Fedha Katika Taasisi zinazopokea Fedha Na kutumia Kama NGO's, Makampuni, Serikali, Watu Binafsi: FundLight
3. Mfumo Wa Kutunza Kumbukumbu Za Mawasiliano Na Nmaba: ContactPedia
4. Mfumo Wa Usimamizi Hospitali:
Mfumo huu ndio uliokuwa mfumo wa kwanza alioutengeneza akiwa mwaka wa mwisho akisomea Computer Science Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam . Aliitwa Tume Ya Taifa Ya Sayansi Na Teknolojia, Tanzania Commission For Science & Technology (COSTECH) kuulezea mfumo huu mbele ya panel na ulikaribia kuchaguliwa katika tuzo kubwa zaidi za Sayansi na Teknlojia (TASTA) nchini Tanzania and It Was Nearly Nominated For High Prize For Science & Technology Award (TASTA Awards) ambapo kipingamizi pekee ilikuwa na kutotumika sehemu yoyote. Unaweza kudownload COSTECH Newsletter Inayoelezea Software Hii Hapa na Taarifa ziko ukurasa wa 3.

Mr. Bukhary Kibonajoro Alichaguliwa Pia Miongoni Mwa Washindi Katika Mpango Mkubwa Wa Ujasiriamali Africa Ujulikanao Kama Tony Elumelu Entrepreneurship Program (TEEP 2015) Kupitia Kutengeneza Kwake Mfumo Wa StraightBook



Unaweza Kumfuata Bukhary Kibonajoro Katika: Facebook, Twitter, LinkedIn, Instagram