English
KUHUSU StraightBook
StraightBook ni mfumo wa usimamizi wa biashara au Uhasibu unaotumiwa katika biashara zaidi ya 1100 Tanzania
na biashara zaidi ya 400 nje ya Tanzania.
Mfumo huu unaweza kutumiwa kwa Kiswahili au English. Unalenga kutumiwa na wafanyabiashara wote wadogo, wa kati na wakubwa
na haijalishi iwapo wanauza huduma au bidhaa au vyote bado mfumo huu utawafaa wote.
Unalenga kuleta mapinduzi katika uendeshaji wa biashara hususan katika bara la Africa ambapo wafanyabiashara wengi
bado wanatunza kumbukumbu kwenye madaftari na kutumia muda mwingi au pesa nyingi katika kupiga mahesabu.
Lakini pia wanapata changamoto katika mamlaka za kodi, mabenki nk kwa kutokuwa na taarifa sahihi za miamala kwenye
biashara zao.
Mfumo huu unaweza kutumiwa katika computer, simu, tablet na hata PDA na mtumiaji anaweza kuutumia popote
atakapokuwa.
Mfumo huo ulitengenezwa kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 2012 na mhandisi wa mifumo ya computer aitwae
Mr. Bukhary Haruna Kibonajoro,
ambae alifanikiwa kuanzisha StraightBook kama kampuni mwaka 2015 ambapo hadi sasa ni Mwenyekiti na Afisa Mkuu Wa Utengenezaji Mifumo
(Chief Technical Officer) wa kampuni hiyo.
Unaweza kuamua kutumia mfumo huu kutokea kwenye internet au ukaamua mfumo huu ufungwe kwenye computer na
kuutumia bila internet.